Skip to main content

Posts

BIASHARA ZA MTAJI USIOZIDI LAKI MOJA!

Recent posts

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...

IFAHAMU ELIMU YA UUAMBAJI BINADAMU BILA KUJAMIIANA (CLONING)

  Mchakato wa uumbaji wa binadamu bila kujaamiana (Cloning) ulianza mwaka 1938 na wanajeshi wa Nazi chini ya kamanda Hitler. Ian Wilmut. Muasisi wa uuambaji wa kondoo aitwaye Dolly, raia wa Uingereza alipata upinzani mkali baada ya kumuumba kondoo huyo akiwa na timu yake ya wanasayansi. Alifariki akiwa na miaka 79 kwa ugonjwa wa kukakamaa yaani "Parkinson's" aliougua kwa muda mrefu, kilieleza chanzo toka Chuo Kikuu cha Edinburg nchini Scotland. Wilmut aliibua mjadala mkali juu ya maadili ya kuwaumba viumbe bila kujaamiana mara alipotangaza kwamba yeye na timu yake ya taasisi ya Baiolojia kwa wanyama ya Roslin wamemuumba mwanakondoo kwa kutumia seli za kiini kutoka kwa kondoo mkubwa, na mwanakondoo huyo akapewa jina la Dolly, kutokana na jina la mwanamuziki Dolly Parton. Uuambaji wa mwanakondoo ulikuwa ni wa awali kwa wanasayansi, kupevusha seli za kiumbe mkubwa na kufanya kazi kama seli za kiumbe mkubwa na kuzaa kiinitete walio sawa. Uumbaji wa Dolly ulianzisha mapinduzi ...

BIASHARA 10 ZA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA KUBWA

  BIASHARA 10 ZA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA KUBWA Tuangalie biashara 20 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000 unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa. Hakuna biashara ndogo, ila kuna biashara unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa. Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo biashara za mtaji mdogo, hebu tuweke sawa kauli ya “zenye faida kubwa”. Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa itakufikisha mbali. ZINGATIA: Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na serikali ambazo unaweza kuzikamilisha bila usumbufu wowote na kwa gharama nafuu sana. Baada ya kulisawaz...

Zijue haki zako kabla na baada ya kukamatwa na askari polisi

  Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, raia ana haki zifuatazo anapokamatwa na askari polisi: 1. Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwake. Mwulize jina lake Mwulize namba yake ya uaskari 2. Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka au kukamatwa. 3. Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa au sehemu anakofanyia kazi kwamba amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa. 4. Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi au Taasisi ya kuzuia rushwa. 5. Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana Iwapo kituo cha polisi au Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika. 6. Raia ana haki ya kuwaeleza polisi au Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu. 7. Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi au Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake. 8. Raia ana haki ya kuyasoma maelezo kabla ya kutia sahihi yake. 9. Raia a...

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Funzo kuhusu vijana na maisha.

  VIJANA WENGI UKIWATIZAMA UTAWAONA KAMA WANA FURAHA LAKINI NYUMA YA PAZIA WANATESEKA SANA NA UMASIKINI. Ni kawaida sana kwa siku hizi kukuta binti wa kike mrembo au kijana wa kiume mtanashati, msomiamemaliza chuo kikuu anamiliki simu kali yaani nzuri sana na yenye gharama kubwa. Wapo pia wanaopendeza kwa nguo nzuri na manukato ya bei kubwa kila utakapowaona huenda hata ukatamani kuwa kama wao. Lakini ukifuatilia nyuma ya pazia hawa vijana wanateseka sana na ugumu wa maisha huku wimbi la ukosefu wa kazi na kipato likizidi kuwatawala. Maumivu wanayopitia ni makubwa mno kuliko unavyoweza kuwaona kwenye sura zao za nje (ambazo ni feki) Kwa isivyo bahati hata wale vijana waliopo vyuo vikuu wanapitia changamoto hii na wala hawajashtuka mapema. Wengi wanakuja kushtuka baadae sana ambapo muda unakua umeshawatupa mkono, Too late!!! Wanaishia kutembeza bahasha za maombi ya kazi kwenye maofisi wanaishia kuonekana kama omba omba tu. Kijana kama unajitambua jitahidi upate maarifa ya biasha...

Elimu kuhusu mikataba ya ajira

  1. NI SHERIA GANI INAYOSIMAMIA MIKATABA AJIRA TANZANIA? Kwa ujumla Sheria ya Mikataba inasimamia aina zote za mikataba Tanzania. Lakini kwa mikataba mahususi kuna sheria mahususi inayosimamia mikataba hiyo. Kwa mfano Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi inaelezea mikataba ya ajira. Kwa maana hiyo ni sawa kusema Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi  ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Mikataba zote zinasimamia mikataba ya ajira.   KUNA AINA NGAPI ZA MIKATABA? Kuna aina kuu tatu (3) za mikataba ambazo unaweza kuajiriwa nayo, nazo ni:  •    Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa: Kama jina linavyojieleza, kwa aina hii ya mkataba kipindi cha ajira hakiainishwi. Mara nyingine huitwa mkataba wa kudumu.  •    Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa: Hii ni aina ya mkataba ambao umetaja kipindi cha muda. Chini ya mkataba huu kama kipindi kilichotajwa kikimalizika basi mkataba utakua umefikia mwisho. Mkataba wa kipindi cha muda uliotajwa u...

Mchezaji aliyesemekana kuumia AFCON aonekana Spain akicheza

 Dakika ya 73 ya mchezo wa kombe la mfalme maarufu kwa jina la Copa Del Rey nchini Hispania kati ya Osasuna na Real Sociedad January 17, Kocha wa Real sociedad alimnyanyua Umar Sadiq kutoka benchi na kumuingiza ili kuchukua nafasi ya Andre Silva. Tukio hilo la staa huyo wa Nigeria liliwashangaza wengi uwanjani kwani mchezaji huyo alikua kwenye kikosi cha timu ya taifa kule Abidjan nchini Ivory Coast akijiandaa kucheza kombe la AFCON 2023. Lakini ikiwa zimebaki siku mbili tu mashindano kuanza, mchezaji huyo alidaiwa kupata majeraha ya goti ambayo yalihitaji afanyiwe upasuaji na angekaa nje kwa zaidi ya wiki tatu, hivyo akapewa ruhusa ya kuondoka kambini. Badala ya kufanyiwa upasuaji kama ilivyotarajiwakatika hali isiyo ya kawaida mchezaji huyo alionekana akicheza kwenye mchezo huo nchini Hispania. Kocha wa Nigeria Jose Peseiro alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alisema ameshangazwa kwa sababu alipokea ripoti kutoka madaktari wa timu ambao walimwambia kwamba staa huyo hatoweza kuru...

Maajabu ya kikongwe wa miaka 72 nchini Moroco

  Leo nimependa kukuletea habari ya kushangaza na yenye kusisimua ya mzee mmoja   wa miaka sabini na mbili (72) anayejihusisha na uuzaji wa vitabu jijini Rabat nchiI Morocco. Huyu mzee anafahamika kwa jina la Mohammed Aziz, licha ya kuwa muuzaji maarufu wa vitabu katika jiji hilo mzee Mohammed amekuwa akishangaza wengi na kuwaacha midomo wazi kwa uwezo wake wa kutumia masaa sita (6) hadi nane (8) kwa siku kusoma vitabu. Akiwa amesoma zaidi ya vitabu 5,000 vilivyo katika lugha ya Kifaransa, Kiarabu na Kiingereza anabaki kuwa muuzaji   mkongwe zaidi ikiwa hadi sasa ana miaka zaidi ya Arobaini na tano (45) katika biashara hiyo akiwa katika eneo hilohilo bila kuhama hata mara moja. Mzee Mohammed anazidi kuwashangaza wengi kwani mzee huyu huacha zaidi ya vitabu 43 nje ambako vingeweza kuibwa lakini hakuna hata kitabu kimoja kinachopotea au kuibiwa. Vyanzo vya habari maarufu nchini humo vilifanya mahojiano nae na kumuuliza kwanini amekua akijiamini kuacha baadh ya vitab...