Skip to main content

Zijue haki zako kabla na baada ya kukamatwa na askari polisi

 


Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, raia ana haki zifuatazo anapokamatwa na askari polisi:

1. Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwake.

Mwulize jina lake

Mwulize namba yake ya uaskari

2. Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka au kukamatwa.

3. Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa au sehemu anakofanyia kazi kwamba amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.

4. Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi au Taasisi ya kuzuia rushwa.

5. Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana Iwapo kituo cha polisi au Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.

6. Raia ana haki ya kuwaeleza polisi au Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.

7. Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi au Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.

8. Raia ana haki ya kuyasoma maelezo kabla ya kutia sahihi yake.

9. Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa au kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.

10. Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.

11. Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

12. Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe

13. Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa:

 (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani,

 (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au 

(c) jirani wa mtu anayetuhumiwa,

14. Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwendendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale. 



Comments

Popular posts from this blog

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...