1. NI SHERIA GANI INAYOSIMAMIA MIKATABA AJIRA TANZANIA? Kwa ujumla Sheria ya Mikataba inasimamia aina zote za mikataba Tanzania. Lakini kwa mikataba mahususi kuna sheria mahususi inayosimamia mikataba hiyo. Kwa mfano Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi inaelezea mikataba ya ajira. Kwa maana hiyo ni sawa kusema Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Mikataba zote zinasimamia mikataba ya ajira. KUNA AINA NGAPI ZA MIKATABA? Kuna aina kuu tatu (3) za mikataba ambazo unaweza kuajiriwa nayo, nazo ni: • Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa: Kama jina linavyojieleza, kwa aina hii ya mkataba kipindi cha ajira hakiainishwi. Mara nyingine huitwa mkataba wa kudumu. • Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa: Hii ni aina ya mkataba ambao umetaja kipindi cha muda. Chini ya mkataba huu kama kipindi kilichotajwa kikimalizika basi mkataba utakua umefikia mwisho. Mkataba wa kipindi cha muda uliotajwa u...
Your number One website to update you with the latest news. This is the home for Politics, Sports, Education and Entertainment news.