Skip to main content

Maajabu ya kikongwe wa miaka 72 nchini Moroco

 

Leo nimependa kukuletea habari ya kushangaza na yenye kusisimua ya mzee mmoja  wa miaka sabini na mbili (72) anayejihusisha na uuzaji wa vitabu jijini Rabat nchiI Morocco.

Huyu mzee anafahamika kwa jina la Mohammed Aziz, licha ya kuwa muuzaji maarufu wa vitabu katika jiji hilo mzee Mohammed amekuwa akishangaza wengi na kuwaacha midomo wazi kwa uwezo wake wa kutumia masaa sita (6) hadi nane (8) kwa siku kusoma vitabu.



Akiwa amesoma zaidi ya vitabu 5,000 vilivyo katika lugha ya Kifaransa, Kiarabu na Kiingereza anabaki kuwa muuzaji  mkongwe zaidi ikiwa hadi sasa ana miaka zaidi ya Arobaini na tano (45) katika biashara hiyo akiwa katika eneo hilohilo bila kuhama hata mara moja.

Mzee Mohammed anazidi kuwashangaza wengi kwani mzee huyu huacha zaidi ya vitabu 43 nje ambako vingeweza kuibwa lakini hakuna hata kitabu kimoja kinachopotea au kuibiwa.

Vyanzo vya habari maarufu nchini humo vilifanya mahojiano nae na kumuuliza kwanini amekua akijiamini kuacha baadh ya vitabu vyake nje ya duka bila kuogopa wezi , alijibu kwa kusema  “Wasioweza kusoma hawawezi kuiba vitabu, na wale wanaojua kusoma siyo wezi.”

Mzee Mohammed anatufundisha kitu kimoja muhimu sana juu ya kupata elimu na maarifa kwa kupitia njia ya usomaji wa vitabu. Alimalizia kwa kusema kuwa katika vitabu kuna maarifa makubwa sana lakini watu wengi haswa waafrika wamekosa tamaduni za kujisomea na badala yake kupoteza muda katika kushiriki mambo mengine ambayo hayana tija yoyote katika maisha yao.

 


Comments

  1. Kibongobongo hata wasomi wenyewe wangemuibia mapema tu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...