Ndugu na Rafiki zangu, nawasalimu katika jina la mwenyezi Mungu. Watu wengi wamekua wakiishi katika mazingira magumu kwa sababu nyingi ikiwemo kukosekana kwa ajira au wengine kuwa na tabia za kuchagua aina ya kazi. Leo Naomba nikushirikishe biashara ambazo unaweza kuzifanya kwa mtaji mdogo tu usiozidi laki moja. Biashara hizi unaweza kuzifanya kama biashara yako rasmi au biashara ya pili(side hustle au chanzo cha ziada cha mapato yako). Lengo, kuingiza faida ya angalau elfu tano kwa siku. 1. Biashara ya genge. Kwa mtaji wa laki moja, utaweza kuwa na bidhaa kama chumvi ya kupima kwenye makopo,vitunguu kwa kuuza reja reja kwa kimoja kimoja au mafungu, nyanya za kuuza moja moja au mafungu, pilipili,tangawizi, mboga za majani, matunda na kadhalika. Amka zako asubuhi nenda hata kujaribu kufanya utafiti wa kawaida tu katika masoko kama vile tandika, stereo, mabibo, buguruni, ilala au soko lolote kubwa ambalo upo karibu nalo, utakuja kugundua kuwa bidhaa zinapatikana kwa bei rahisi sana,...
Your number One website to update you with the latest news. This is the home for Politics, Sports, Education and Entertainment news.