Skip to main content

BIASHARA ZA MTAJI USIOZIDI LAKI MOJA!

Ndugu na Rafiki zangu, nawasalimu katika jina la mwenyezi Mungu. 

Watu wengi wamekua wakiishi katika mazingira magumu kwa sababu nyingi ikiwemo kukosekana kwa ajira au wengine kuwa na tabia za kuchagua aina ya kazi.

Leo Naomba nikushirikishe biashara ambazo unaweza kuzifanya kwa mtaji mdogo tu usiozidi laki moja. Biashara hizi unaweza kuzifanya kama biashara yako rasmi au biashara ya pili(side hustle au chanzo cha ziada cha mapato yako).

Lengo, kuingiza faida ya angalau elfu tano kwa siku.

1. Biashara ya genge.

Kwa mtaji wa laki moja, utaweza kuwa na bidhaa kama chumvi ya kupima kwenye makopo,vitunguu kwa kuuza reja reja kwa kimoja kimoja au mafungu, nyanya za kuuza moja moja au mafungu, pilipili,tangawizi, mboga za majani, matunda na kadhalika. Amka zako asubuhi nenda hata kujaribu kufanya utafiti wa kawaida tu katika masoko kama vile tandika, stereo, mabibo, buguruni, ilala au soko lolote kubwa ambalo upo karibu nalo, utakuja kugundua kuwa bidhaa zinapatikana kwa bei rahisi sana, hivyo unaweza kununua na ukaja kuuza nyumbani ukajipatia faida nzuri tu.

2. Biashara ya mayai.

Laki moja kwa watu walio katika miji na hata walio nje ya miji, kwa kiasi cha shilingi laki moja unaweza kupata trei kumi kwa wastani elfu tisa yaani yai moja umelinunua kwa mia tatu ukizileta mjini utapata faida ya kila trei elfu mbili.

Lakini pia, unaweza kutafuta vijana,ukachemsha mayai kila mmoja ukampatia trei moja akauze kwa mia tano mia tano, halafu unampatia elfu moja na mia tano baada ya trei kuisha,kwa maana unampatia nafasi kwani u-sharp wake ndiyo utakaomsukuma kupata 1,500 nyingi Zaidi.

3. Biashara ya kuku wa kienyeji.

Pita majumbani (Vijijini nan je ya miji inapendeza zaidi). Utapata kuku wakubwa wa kienyeji Saba mpaka nane lakini hii itategemea zaidi uko mkoa gani. Utakayemnunua kwa kumi na mbili uza kumi na tano,utakayemnunua kwa kumi na tano uza ishirini. Kwa watu walioko mkoa wa Kigoma, Vijijini Kuna kuku wa elfu saba kijijini, mjini unauza elfu kumi. Jamani si mnaona kuku wanavyoliwa sana kwenye miji? Sasa unasubiri nini Rafiki yangu? Changamkia fursa hiyo.

4. Biashara ya matunda ya kutembeza.

Yenyewe elfu hamsini inatosha cha muhimu uwe na deli lako. Nunua matikiti na nanasi, menya na kata vipande vipande, uza vipande mia tatu na mia tano kwa kutegemea na ukubwa wa tikiti lako. Muhimu usiwe mvivu wa kutembea. Kwa wanaume mara nyingi hutumia Baiskeli, unalangua mananasi unatafuta center unaenda unamenya mananasi na kuuza kwa vipande au reja reja.

5. Biashara ya mikoba.

Kuna mikoba ya kike jumla Kariakoo ni elfu kumi na moja kwa mikoba Kumi. Mkoba mmoja utauza kwa reja reja ishirini wakikupunguza sana elfu kumi na tano. Hii unaweza kuiposti katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, Instagram, twitter, tiktok na whatsp status ukauza pia. Niliwahi kufanya tafiti nikagundua kuwa siyo kila mtu anapenda kutembea kwenye masoko au maduka kutafuta bidhaa kutokana na changamoto za mud ana usumbufu, Hivyo kuna fursa kubwa sana ya wewe kupata wateja wako kwa njia ya mtandao tu. Unaweza kufanya hata bila ya kuwa nae neo la biashara.

6. Biashara ya viatu vya kike

Kuna simple na ndala za kike unanunua jumla elfu nne mia tano unauza elfu saba au nane, unanunua elfu tano unauza mpaka elfu kumi(Biashara hii hata mimi naifanya). Unaweza pia kuifanya kwa kuposti status.

7. Biashara za viatu vya watoto wadogo na wachanga.

Haitofautiani sana na viatu vya kike vya wazi huviita simple, unanunua elfu tano unauza elfu kumi kwa reja reja lakini inatakiwa uwe vizuri kuchagua kiatu kizuri. Kuna vya watoto wachanga kabisa vinauzwa elfu tano, bei ya kununua mara nyingi huwa ni elfu tatu. Hata mimi pia naifanya. Kwa WhatsApp status pia unauza.

8. Biashara ya mbuzi wa kienyeji.

Unaweza kupita majumbani kutafuta mbuzi, kijijini inapendeza zaidi. Laki moja unanunua mbuzi wawili wa elfu hamsini hamsini ambao unaweza kuwauza sitini hadi sabini itategemea uzoefu wako wa kupunguzisha bei. Majike yanapendwa zaidi na wachinjaji na wauza supu ya mbuzi kuliko madume, lakini pia usinunue mbuzi wa kufugwa bandani wanakonda sana hautapata bei nzuri ndiyo maana nikashauri uende kijijini. Biashara hii ni ngumu kama haujui kupunguzisha bei na kuongea, kadri unavyokuwa mzoefu ndivyo unavyotengeneza faida lakini hauwezi kupata uzoefu pasipo kuanza. Anza sasa!

Kwa leo katika "Biashara ni utajiri" tuishie hapa! Unaweza kubonyeza link hapo chini kujiunga na whatsp group kupata elimu Zaidi.

https://chat.whatsapp.com/Kb7EFiAfQEH3hHi9mJsu6D?mode=ac_t

Haki Zote Zimehifadhiwa

©️ 2025 MOPAO MEDIA


Comments

Popular posts from this blog

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...