Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2024

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Funzo kuhusu vijana na maisha.

  VIJANA WENGI UKIWATIZAMA UTAWAONA KAMA WANA FURAHA LAKINI NYUMA YA PAZIA WANATESEKA SANA NA UMASIKINI. Ni kawaida sana kwa siku hizi kukuta binti wa kike mrembo au kijana wa kiume mtanashati, msomiamemaliza chuo kikuu anamiliki simu kali yaani nzuri sana na yenye gharama kubwa. Wapo pia wanaopendeza kwa nguo nzuri na manukato ya bei kubwa kila utakapowaona huenda hata ukatamani kuwa kama wao. Lakini ukifuatilia nyuma ya pazia hawa vijana wanateseka sana na ugumu wa maisha huku wimbi la ukosefu wa kazi na kipato likizidi kuwatawala. Maumivu wanayopitia ni makubwa mno kuliko unavyoweza kuwaona kwenye sura zao za nje (ambazo ni feki) Kwa isivyo bahati hata wale vijana waliopo vyuo vikuu wanapitia changamoto hii na wala hawajashtuka mapema. Wengi wanakuja kushtuka baadae sana ambapo muda unakua umeshawatupa mkono, Too late!!! Wanaishia kutembeza bahasha za maombi ya kazi kwenye maofisi wanaishia kuonekana kama omba omba tu. Kijana kama unajitambua jitahidi upate maarifa ya biasha...