VIJANA WENGI UKIWATIZAMA UTAWAONA KAMA WANA FURAHA LAKINI NYUMA YA PAZIA WANATESEKA SANA NA UMASIKINI.
Ni kawaida sana kwa siku hizi kukuta binti wa kike mrembo au kijana wa kiume mtanashati, msomiamemaliza chuo kikuu anamiliki simu kali yaani nzuri sana na yenye gharama kubwa. Wapo pia wanaopendeza kwa nguo nzuri na manukato ya bei kubwa kila utakapowaona huenda hata ukatamani kuwa kama wao.
Lakini ukifuatilia nyuma ya pazia hawa vijana wanateseka sana na ugumu wa maisha huku wimbi la ukosefu wa kazi na kipato likizidi kuwatawala. Maumivu wanayopitia ni makubwa mno kuliko unavyoweza kuwaona kwenye sura zao za nje (ambazo ni feki)
Kwa isivyo bahati hata wale vijana waliopo vyuo vikuu wanapitia changamoto hii na wala hawajashtuka mapema. Wengi wanakuja kushtuka baadae sana ambapo muda unakua umeshawatupa mkono, Too late!!! Wanaishia kutembeza bahasha za maombi ya kazi kwenye maofisi wanaishia kuonekana kama omba omba tu.
Kijana kama unajitambua jitahidi upate maarifa ya biashara uanze kujenga biashara yako, haya mambo ya kusubiria kuajiriwa ni utumwa, tena ni utumwa uliopitiliza.
Wewe kama kijana unajitambua na unatamani kuondokana na hali hii ya maisha feki ya kuonekana uko vizuri kimaisha kumbe shida zimekujaa usisite kuwasiliana nami, nitakufundisha namna ya kuweza kujipatia kipato na kujikomboa kutoka umaskini. Endelea kufuatilia Mopao media kwa elimu zaidi juu ya maisha.

Comments
Post a Comment