Skip to main content

Mchezaji aliyesemekana kuumia AFCON aonekana Spain akicheza

 Dakika ya 73 ya mchezo wa kombe la mfalme maarufu kwa jina la Copa Del Rey nchini Hispania kati ya Osasuna na Real Sociedad January 17, Kocha wa Real sociedad alimnyanyua Umar Sadiq kutoka benchi na kumuingiza ili kuchukua nafasi ya Andre Silva.



Tukio hilo la staa huyo wa Nigeria liliwashangaza wengi uwanjani kwani mchezaji huyo alikua kwenye kikosi cha timu ya taifa kule Abidjan nchini Ivory Coast akijiandaa kucheza kombe la AFCON 2023. Lakini ikiwa zimebaki siku mbili tu mashindano kuanza, mchezaji huyo alidaiwa kupata majeraha ya goti ambayo yalihitaji afanyiwe upasuaji na angekaa nje kwa zaidi ya wiki tatu, hivyo akapewa ruhusa ya kuondoka kambini.

Badala ya kufanyiwa upasuaji kama ilivyotarajiwakatika hali isiyo ya kawaida mchezaji huyo alionekana akicheza kwenye mchezo huo nchini Hispania.

Kocha wa Nigeria Jose Peseiro alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alisema ameshangazwa kwa sababu alipokea ripoti kutoka madaktari wa timu ambao walimwambia kwamba staa huyo hatoweza kurudi kwenye hali yake na alihitaji angalau siku 14 ili kuwa fiti.

Comments

Popular posts from this blog

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...