Skip to main content

BIASHARA 10 ZA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA KUBWA

 BIASHARA 10 ZA MTAJI MDOGO ZENYE FAIDA KUBWA

Tuangalie biashara 20 za mtaji mdogo usiozidi Tshs. 100,000 unazoweza kufanya na zenye faida kubwa. Mtaji mkubwa unaohitajika unapoanzisha biashara ni muda na wala sio pesa kama utakavyojifunza hapa.
Hakuna biashara ndogo, ila kuna biashara unazoweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa. Hiyo ambayo inaitwa “biashara ndogo” ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku itakutoa.
Kabla hatujaenda kwenye hiyo orodha ya hizo biashara za mtaji mdogo, hebu tuweke sawa kauli ya “zenye faida kubwa”. Faida kubwa haimaanishi mamilioni ya fedha, bali ni kwamba faida utakayoipata kulingana na mtaji wako ni nzuri na usipokata tamaa itakufikisha mbali.

ZINGATIA:
Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile, ni vyema kufuatilia utaratibu na sheria za mahali ulipo. Tafadhali ilinde biashara yako kwa kufuata kanuni zote zilizowekwa na serikali ambazo unaweza kuzikamilisha bila usumbufu wowote na kwa gharama nafuu sana.
Baada ya kulisawazisha hilo, twende kwenye hiyo orodha ya biashara za mtaji mdogo kama zifuatazo;

1. KUPIKA KWA ODA
Kama wewe ni mpishi mzuri au una mtu anayejua kupika, basi jitangaze kama unapokea oda za mapishi fulani. Tuchukulie unaweza kupika makande au wali nyama vizuri.
Unachoweza kufanya ni kwenda maofisi ya karibu yako na kuwaambia kwamba wakutafute wanapohitaji hicho chakula wakati wa mchana na wewe utawaletea. Usisahau kuacha mawasiliano yako ili waweze kukutafuta. Wengi wao watapenda hiyo huduma kwasababu hawatohitaji kutoka tena kufata chakula.

2. UREMBO (MAKEUP, KUSUKA & KUCHA)
Urembo ni gharama. Wanadada wanataka kupendeza wanapokwenda safari zao kama ni kazini ama shughulini. Uzuri ni kwamba hii ni biashara ya kila siku unayoweza kufanya. Baada ya kufanya utafiti wangu, nimebaini kwamba kufanya makeup, kutengeneza kucha na ususi wa nywele zinalipa vizuri tu. Kuna watu wengi tu wanaendesha maisha yao kupitia biashara hizo. Kwanini wewe ushindwe? Na kama sio mtaalamu, hakuna tatizo. Chukua muda wako na kujifunza, ndani ya muda utaweza.

3. KUUZA JUISI NA ICECREAM
Kujifunza kutengeneza juisi au icecream haitakuchukuwa muda mrefu. Ili kufanikiwa katika biashara hii, cha muhimu ni kujitofautisha. Muhimu zaidi unapofanya biashara ya kutengeneza juisi au icecream, ni kuweka mazingira yako safi na salama kwa wateja wako. Uzuri wa biashara hii ni kuwa mtaji wake ni mdogo sana. Elfu kumi tu inatosha kuanzia na wapo waliofanya hivyo na wamekuza biashara zao kama vile Mak Juice au Zanana Juice Box.

4. KILIMO CHA MBOGAMBOGA
Kilimo ni sehemu kubwa ya maisha ya watanzania na wale wa nchi nyingi za Afrika. Kila siku zikienda, kilimo huzidi kuwa ni biashara ya matajiri kwasababu shamba lina gharama kubwa. Licha ya hivyo, bado kuna fursa ya kutengeneza kipato kupitia kilimo cha mbogamboga hata kama una mtaji mdogo. Anza na sehemu ndogo tu unayoweza kupata hata kama ni nyumbani.

5. UFUGAJI WA NDEGE (KUKU, BATA, N.K)
Hii ni biashara ambayo ina faida kubwa lakini pia ina changamoto zake kama vile kuku wako kufa. Vifo vya mifugo huwaumiza sana wafugaji na mara nyingi husababishwa na mifugo hiyo kula uchafu. Hivyo, unapoingia kwenye ufugaji jitahidi uwe na mazingira safi na salama kwa mifugo yako. Usafi wa mara kwa mara hasa hasa kwenye malisho yao utahitajika. Kwa vile mtaji ni mdogo, unaweza kuanza na kuku wa kienyeji, bata au hata njiwa. Japo kuwa wanachukuwa muda ila kuwa mvumilivu, faida utaiona.

6. KUTENGENEZA TOVUTI (WEBSITES)
Tuko katika ulimwengu wa habari na teknolojia, hivyo kampuni ama biashara ambayo hawako mtandaoni wanakosa wateja. Ichangamkie fursa hiyo kwa kujifunza kutengeneza websites kupitia YouTube. Kisha, tafuta biashara/ makampuni ambayo hawana tovuti na uwaelezee umuhimu wa kuwa na tovuti. Mwisho, waambie kuwa wewe unatoa huduma hiyo. Kwa kuanza, wateja wako wa mwanzo unaweza kuwafanyia kwa bei ya punguzo halafu mbeleni ukapandisha. Njia hii itakusaidia kupata mabalozi watakao kupatia wateja wengine.

7. KUPANGA SHEREHE/MATUKIO (EVENT PLANNING)
Kuanzia maharusi, kitchen party, send - off na sherehe nyenginezo nisizozifahamu. Zote hizi ni fursa ambapo unaenda kusaidia watu kuandaa sherehe zao mwanzo mpaka mwisho. Wewe ndio unaumiza kichwa kutafuta watu na huduma mbalimbali kama vile wapambaji, ma DJ, au kuwatafutia gari ya kukodi, kuwapikia chakula na megine mengi. Unachohitaji kuweza kufanya biashara hii ni uwe unawajua watu husika wanaotakiwa kwenye sherehe hizo. Mfano, ujue wapambaji wa ukumbi, wapishi wa maharusi, ma-DJ ili uweze kuwapa kazi hizo. Utalipwa kwa kufanya kazi hiyo.

8. USHONAJI NGUO
Kama wewe ni mpenzi wa mitindo, unaweza tengeneza kipato kizuri kwa kuwashonea watu nguo. Itakuchukuwa muda kujifunza kushona ila ni kazi moja nzuri. Unapata kuwa mbunifu katika kutengeneza mishono mbali mbali na mwisho wake kulipwa. Kama huna cherehani nyumbani, unaweza kwenda kukodi na kufanyia kazi zako hadi utakapo nunua yako.

9. KUFUNDISHA
Unaweza kufundisha chochote kila unachokijua ikiwa kuna watu wanataka kujifunza. Jitathmini kwa kujiuliza, je ni kitu gani nakijua ambacho watu wanataka kujifunza? Hiyo ni rasilimali tosha. Watafute hao watu na uwape huduma zako. Taaluma sio lazima iwe kufundisha hesabati na kemia tu, kama unajua kupika vizuri, kushona au chochote kile basi wafundishe watu.

10. KUNUNUA NA KUUZA BIDHAA
Sifa ya kubwa ya mjasiriamali ni kuona thamani ya vitu kabla wengine hawajaviona. Hivyo, tafuta bidhaa ambazo zinauzwa kwa bei ya chini, zinunue na utafute soko ambalo hizo bidhaa zinauzwa kwa bei ya juu uende ukaziuze huko. Mfano, unaweza kutoa bidhaa Dar es Salaam ukaenda kuuza Mwanza na kinyume chake pia inawezekana.

Kama nilivyotangulia hapo awali kwa kusema; “hakuna biashara ndogo”. Kinachofanya biashara ifanikiwe sio pesa, ni kujifunza, bidii, mbinu na kutokata tamaa katika safari yako hiyo. Jasho na muda ndio mtaji mkubwa na kila kizuri kina changamoto zake. Hivyo, changamoto zitakapokuja kuwa na ujasiri wa kutafuta suluhisho lake. Ukiweza kufanya hivyo utapiga hatua. Amua kwa Busara. Karibu kwenye page yetu tujifunze masuala anuwai kuhusu Mahusiano, Biashara na maisha kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

  Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa. 1) DHAMBI. Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,t ulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31   lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.  2) KUKOSA IMANI. Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa  inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao. Wa e brania 11:6  Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana m...

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...