Skip to main content

Kwanini Mungu hajibu maombi yetu?

 


Wakati mwingine tumekuwa tukiomba sana kwa Mungu lakini hatupokei majibu. Leo tutajifunza mambo 10 yanayosababisha maombi yetu kutojibiwa.

1) DHAMBI.
Baada ya mwanadamu kuasi pale Eden dhambi iliingia ulimwenguni na kila aliyezaliwa alikua na dhambi. Lakini hii haikumaanisha kwamba tukiomba Mungu hatusikii, bali ilimaanisha ili Mungu atusikie,tulipaswa kwanza kutubia makosa na dhambi zetu ndipo tumueleze Mungu matatizo yetu.
Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.


Yohana 9:31 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
Hivyo basi kabla hujampelekea Mungu matatizo/shida yako hakikisha mahusiano yenu yako vizuri.

 2) KUKOSA IMANI.
Nadhani hii ni miongoni mwa sababu kubwa inayofanya watu wasipokee majibu ya maombi yao.

Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

’Hapa ni mchezo wa akili yako na nafsi yako juu ya Mungu unayemuomba na kile unachomuomba. Wakati Yesu alipokuwa anaponya watu, mara nyingi sana aliwaambia ‘Imani yako imekuponya

’(Luka 17:19) kwahiyo imani ndio msingi wa majibu ya maombi yako kwa Mungu.
Kiwango cha imani yako ndio kitaamua kiasi cha majibu yako kwa Mungu.


3) KUKATA TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Kuna wakati unaweza kusikia mtu akisema, nimeomba vya kutosha Mungu hanisikii, labda Mungu hanioni. Kauli zote hizi za kukata tamaa hufanya tushindwe kupokea majibu ya maombi yetu. Habakuki aliambiwa ‘njozi ni kwa wakati ulioamriwa, na ijapokawia aingojee.
Habakuki 2:2-3

Na muda mwingine majibu yetu yanakuwa yamebeba vitu vikubwa hivyo hukumbana na upinzani mkali, bila kukazana kuomba basi hushindwa kutufikia. Maombi ya Daniel yalizuiliwa kwa siku 21 na mkuu wa anga wa uajemi, kama angekata tamaa basi asingepata majibu ya maombi yake. Daniel 10:12-13.

4) KUJIKWEZA/KUJIHESABIA HAKI.
Kuna baadhi ya watu hujiona kama vile wao ni zaidi ya watoto wa Mungu na wana haki zote na hawana dhambi na ni lazima wapewe kila wanachokiomba. Kama una tabia hiyo, my friend Mungu hatojibu maombi yako, maana Biblia inasema ajikwezaye atashushwa. 
Luka 14:11


Yesu aliwahi kutoa mfano wa mfarisayo na mtoza ushuru, mfarisayo alikihesabia haki alafu mtoza ushuru akajishusha na kujiona mdhambi. Yesu anasema mtoza ushuru alihesabiwa haki kuliko mfarisayo...

5) KUOMBA BILA KUFANYA KAZI.
Unakuta mtu anaomba Mungu ampe kazi alafu anashinda nyumbani tu bila kutafuta kazi. My friend, Biblia inasema asiyefanya kazi na asile, kwaiyo kama hufanyi kazi hata kama unamuomba Mungu hawezi kukubariki/kukujibu maana Mungu anabariki kazi za mikono yetu. Sasa atabariki nini kama hufanyi kazi?  Zaburi 128:2, na  2Thesalonike 3:10
Kuna wakati siyo kuomba tu, lazima kuambatane na kutafuta na kubisha, ili uweze kuona na kufunguliwa. 
 Luka 11:9

6) KUTOSAMEHE.
Ndiyo! Kutosamehe waliokukosea ni sababu mojawapo ya kuzuia majibu ya maombi yako. Maana ili Mungu aweze kukusamehe na kukusikiliza inapaswa kwanza uwasamehe wengine kama Yeye anavyokusamehe.
 Efeso 4:32, Mathayo 6:12-15

7) KUOMBA NJE YA MAPENZI YA MUNGU.

Kuomba nje ya mapenzi ya Mungu ni kuomba nje ya utaratibu wa Mungu au kuomba nje ya mipango ya Mungu aliyokuwekea juu ya maisha yako. Utajuaje kama unaomba nje ya mapenzi ya Mungu? ( Tuombe uzima Mungu akinipa kibali nitaandika)1Yohana 5:14


8) KUTOAMBATANISHA NA SADAKA.

Siku hizi ukigusa ishu ya sadaka tu, watu wanakuwa wakali kama pilipili. Lakini hiyo haiondoi ukweli wa kuwa sadaka ni muhimu sana katika maombi yako. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. ‘Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.’ Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote .Zaburi 20:2-4


Na ukisoma kwenye Biblia sadaka ni kitu cha lazima, ili kuonyesha utii wako mbele ya Mungu. Lakini hamaanishi basi ukiambatanisha na sadaka unajibiwa, kumbuka sadaka ya mtu mwovu ni chukizo mbele za Mungu.  Mithali 15:8 Japokuwa sadaka ya kwanza ni moyo wako, na ya pili ni Damu ya Yesu. Hivyo kama huna sadaka unaweza tumia hizo mbili na Mungu akajibu maombi yako kwa wakati na bila shida.

9) KUTAKA KUTUMIA KWA TAMAA.
Wakati mwingine hatupokei majibu ya maombi yetu kwa kuwa lengo letu tukipata ni ili kumtambia fulani, kumuumiza fulani, kufanyia anasa za dunia nk. Sasa ukiwa na nia hiyo moyoni mwako Mungu hakujibu. Yakobo 4:3


10) KUTOMKUMBUSHA MUNGU.
Kumkumbusha Mungu haimaanishi kwamba Mungu anasahau, bali kuna wakati anapenda Uungu wake uheshimiwe kwa sisi kumkumbusha ahadi yake kwetu na siyo kukaa tu na kusubiri majibu.

Isaya 43:26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.


Huenda maombi yako yako mlangoni pako, ni kiasi tu cha kwenda mbele za Mungu kumkumbusha na kumshukuru nawe utapokea. 

Kama umependa mafundisho haya na unataka kujifunza mengi zaidi bonyeza link hapa chini ujiunge na group la whatsapp - https://chat.whatsapp.com/D3QWYtaZ0864OxdUYSOCUXAsante na Ubarikiwe sana.

IMETOLEWA NA PASTOR ALFA & DANIEL – CHURCH OF CHRIST - MAJOHE

 


Comments

Popular posts from this blog

Nyumba ya P.Diddy yavamiwa na maafisa usalama

  Nyumba ya mfanyabiashara na mwanamuziki maarufu nchini Marekani P.Diddy ambaye sasa hivi anajiita DIDDY imevamiwa na maafisa wa usalama wa nchini Marekani kwa ajili ya upekuzi na uchunguzi. Maafisa wa usalama hao walivamia nyumba ya Diddy na kuwafunga pingu watoto wake wawili wanaofahamika kwa majina ya King na Justin wakati huo huo baba yao ikiwa hajulikani alipo. Inasemekana mara ya mwisho ndege ya Diddy ilikuwa ikionekana angani kuelekea visiwa vya Carribean. Diddy anashutumiwa kujihusisha na biashara haramu za ngono na biashara ya binadamu na hii ndiyo sababu uvamizi huo umefanyika katika nyumba yake. 

Imamu shoga auliwa na wasiojulikana

  M uhsin Hendricks, mtu mashuhuri aliyejulikana kama imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ameuwa kwa risasi nchini Afrika Kusini. Kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 57 alikuwa anaongoza msikiti mmoja katika jijini la Cape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa waumini wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii. Alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa. "Washukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari ingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hilo," polisi walisema katika taarifa yao. Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Julia Ehrt, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Internati...